Diddy akalia kuti kavu, polisi wamdaka

Diddy akalia kuti kavu, polisi wamdaka

Mkali wa Hip Hop kutoka Marekani Diddy ameripotiwa kukamatwa na polisi New York kufuatia tuhuma za kujihusisha na unyanyasaji wa ngono na biashara za madawa ya kulevya.


Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali nchini Marekani ikiwemo CNN na TMZ zinaeleza kuwa Diddy alikamatwa katika mitaa ya Manhattan huku chanzo cha karibu cha polisi kikidai kuwa alitakiwa kukamatwa leo Jumanne Septemba 17,2024 lakini mamlaka iliamuru akamatwe usiku wa kuamkia leo.

Mbali na hayo mwanasheria wa Diddy, Marc Agnifilo amesikitishwa na uamuzi huo huku akidai kuwa Diddy siyo mkamilifu lakini sio muhalifu hivyo amepanga kulisafisha jina lake mahakamani.


“Yeye ni mtu asiyekamilika lakini si mhalifu. Kwa sifa yake Bw. Combs amekuwa akishirikiana na uchunguzi huu na kwa hiari yake alihamia New York wiki iliyopita kwa kutarajia mashtaka haya. Tafadhali hifadhi hukumu yako hadi utakapokuwa na mambo yote haya ni matendo ya mtu asiye na hatia asiye na la kuficha, na anatazamia kusafisha jina lake mahakamani” Marc ameambia TMZ

Utakumbuka kuwa Diddy ameanza kuhusishwa kwenye kesi za unyanyasaji wa kingono mwishoni kwa mwaka jana baada ya wanawake kadhaa kwenda kushitaki kufanyiwa ukatili na Combs akiweno aliyekuwa mpenzi wake Cassie.

Kufuatia na hayo mapema mwaka huu Machi 25 makazi ya msanii huyo ya Los Angeles na Miami yalipigwa msako na mamlaka wa usalama wa Taifa.

Mbali na msako huo Mei 17 mitandao ya kijamii iliibuka tena baada ya video ya Diddy akimpiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie hotelini tukio lililotokea mwaka 2016, hata hivyo Combs kupitia Instagram yake aliomba radhi kufuatia na video hiyo huku akidai kuwa kwa wakati huo hakuwa sawa kiakili.


Aidha mpaka kufikia sasa Diddy anahusishwa kwenye kesi nane tofauti tofauti huku nyingi zikidaiwa kuwa za unyanyasaji wa kingono huku akipokonywa baadhi ya heshima alizotunukiwa ikiwemo Shahada ya Chuo Kikuu cha Howard, Orodha ya ngoma kushuka kwa mujibu wa Billboard, kampuni ya Diageo kusitisha mkataba, miwani zenye saini yake kusitishwa kuuzwa na mengineyo mengi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags