Akon Na Mchango Wake Kwenye Afrobeat

Akon Na Mchango Wake Kwenye Afrobeat

Mwanamuziki na mwigizaji kutoka Senegal ambaye anaishi Marekani, Akon amefunguka kuhusu mchango wake katika kukuza muziki wa Afrobeat na namna ambavyo amepambana na changamoto kuutambulisha muziki huo Kimataifa.

Wakati alipokuwa kwenye moja ya mahojiano yake ya hivi karibuni aliweka wazi alijaribu kuwasilisha muziki wa Afrobeat katika kampuni za kurekodi nchini Marekani lakini walimkatalia kumsapoti.

“Nakumbuka huko nyuma mwanzoni mwa miaka ya 2000, nilipokuwa nikijaribu kutafuta soko na kupata saini ya Afrobeats huko Marekani, walidhani ni muziki wa Reggae. Ilikuwa moja ya mambo ambayo yalikuwa ya kukatisha tamaa, kujaribu kuwafanya waelewe idadi ya Waafrika ilikuwa kubwa, na muziki huu utakuwa siku zijazo. Kwa bahati mbaya, nilipata shinikizo kubwa.

Afrobeats itakuwepo kwa muda mrefu, kwa sababu imekuwepo kwa muda mrefu [tayari]. Jukumu ambalo nililifanya kwa kweli lilikuwa kusaidia kuifichua, kuiweka nje, na kutumia kila fursa niliyokuwa nayo, na kila uhusiano niliokuwa nao, kila rasilimali niliyokuwa nayo, kuitambulisha na kutumaini kwamba watu watavutiwa,” alisema Akon

Katika juhudi zake za kukuza muziki wa Afrika, Akon alieleza kuwa alimsaini Wizkid kwenye lebo yake ya ‘Konvict Music’ mwaka 2008, na alishirikiana na wasanii wengine kama P-Square na Davido.

Aidha msanii huyo anaamini kuwa muziki wa Afrobeats utaendelea kuwepo kwa muda mrefu na utaendelea kuwa chombo cha kuutangaza utamaduni wa Afrika duniani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags