Wanamuziki wa Bongo Fleva nchini Diamond Platnumz na Zuchu huwenda wakawa wamemaliza tofauti zao, hii ni baada ya wawili hao kuonekana kuwa karibu zaidi siku ya jana Februari 7, 2025 katika sherehe ya harusi ya msanii mwenzao Jux.
Kufuatia na video zinazoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii zimekuwa zikipokea maoni tofauti tofauti huku wengi wao wakimpongeza Zuchu kuchukua uamuzi mzuri wa kuamua kurudiana na Simba na wengine kumkosoa msanii huyo.
Utakumbuka kuwa ugomvi wa wawili hao walianza mwezi ulioisha huku ukichochewa zaidi kuhusiana na suala zima la Zuchu kudaiwa kulazimisha kuolewa na Simba jambo ambalo lilipelekea Zuchu kutuma barua ya wazo kwa Simba kutokana na mambo anayofanyiwa na watangazaji wake ambayo yalikuwa yakimuumiza kiakili na kihisia.
Mbali na hilo lakini pia msanii huyo alichukuwa jukumu la kuondoa utambulisho wa kuwa yeye ni msanii wa lebo ya WCB ambapo mpaka kufikia sasa hajarudisha utambulisho huo licha ya wawili hao kuonekana kuwa na maelewano mazuri kwa siku za hivi karibuni.
Aidha ukiachana na wawili hao kuwa kwenye mahusiano na kupitia migogoro kadhaa lakini wamewahi kutoa ngoma za pamoja ikiwemo Wale Wale, Mtasubiri, Raha, Cheche na nyinginezo.

Leave a Reply