Diamond ataja sababu kupangwa mchana show ya Afronation

Diamond ataja sababu kupangwa mchana show ya Afronation

Mkali wa ngoma ya ‘Komasava’ Diamond amefunguka kuhusu suala la waandaji wa Tamasha la ‘Afronation’ linalifanyika nchini Ureno kumpanga mchana tofauti na wasanii wengine kutoka mataifa mbalimbali.

Diamond ametoa sababu hiyo kupitia instastory yake kwa kuandika kuwa wanafanya hivyo kwasababu ni show zao hivyo lazima wawape kipaumbele wasanii wao.



“Najua mnachukizwa na muda wanaotupanga kwenye show ila uhalisia hizi show zao hivyo lazima wajipe vipaumbele lakini pia lazima tukubali ya kuwa wenzetu walitutangulia kwenye kufanya matukio na ngoma za kidunia, sisi ndio tumeanza ila amini ya kwamba muda sio mrefu kila kitu kitabadilika kikubwa naombeni tuu muendelee kunisapoti na kuniombea harafu angalieni sinema” ameandika Diamond

Utakumbuka kuwa jana jioni mwanamuziki Diamond alipanda jukwaani katika tamasha la ‘Afronation’ na kutumbuiza ngoma zake ikiwemo ‘Shu’ na ‘Komasava’.

Mastaa wengine ambao wameshaonesha mbwembwe zao katika jukwaa hilo ni pamoja na Rema, Nicki Minaj, Fally Ipupa, Tyla na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags