CR7 kuchapwa viboko 99

CR7 kuchapwa viboko 99

Nguli wa ‘soka’ kutoka nchini Portugal Cristiano Ronaldo amejikuta katika janga ambalo hakulitegemea baada ya vyombo vya habari nchini Iran kuripoti kuwa mchezaji huyo amehukumiwa kuchapwa viboko 99 kwa kosa la uzinzi pindi ambapo atakanyaga nchini Iran.

Kwa mujibu wa TMZ imeeleza kuwa taarifa hizo zimekuja baada ya mchezaji huyo kupata mapokezi ya aina yake nchini humo wakati Al Nassr ilipocheza na Persepolis katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Asia ambapo kama sehemu ya ukaribisho wa Ronaldo alipewa zawadi kutoka kwa mashabiki wanaompenda, ikiwa ni pamoja na michoro yenye picha zake.

Katika kumshukuru Fateme ambaye ni mchoraji wa zawadi yake , Ronaldo alikumbatiana na kumbusu shavuni, jambo ambalo liliwakasirisha kundi la wanasheria wenye msimamo mkali wa kidini nchini Iran kwa sababu chini ya sheria za Iran, kumgusa mwanamke ukiwa haujamuoa ni aina uzinzi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags