Nyota wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Al-Nassr, ameripotiwa kuwa huwenda akashiriki Kombe la Dunia mwaka 2030.
Kwa mujibu wa mchezaji mwenzake aitwaye ‘Nani’ ameeleza kuwa CR 7 amepanga kuboresha mtindo wake wa lishe kwa ajili ya Kombe la Dunia 2030.
Ikumbukwe kuwa 2030 Ureno itakuwa mwenyeji mwenza wa mashindano hayo pamoja na Hispania na Morocco, ushiriki wa Ronaldo hautakuwa tu tukio la kihistoria bali pia litaheshimu taaluma yake ambapo kufikia mwaka huo atakuwa na miaka 45.
Leave a Reply