BREAKING NEWS: Mzee wa “Buga”, Kizz Daniel atiwa mbaroni Dar

BREAKING NEWS: Mzee wa “Buga”, Kizz Daniel atiwa mbaroni Dar

Msanii maarufu kutoka Nigeria 🇳🇬 anayetamba kwa nyimbo ya "Buga," Kizz Daniel ametiwa mbaroni leo hii baada ya kushindwa kufika na kuperform stejini usiku wa kuamkia leo katika tamasha la Summer Amplified.


Kama tulivyowadokezea hapo awali, msanii huyo alipaswa kupanda stejini kwenye mida ya saa tisa usiku, ila haikutokea hivyo, kitendo kilochowafanya watu kupata hasira kali na kuanzisha fujo.


Ikumbukwe kuwa waTanzania walitoka walitoka sehemu mbalimbali, wapo waliosafiri kutoka mikoa ya mbali ili kuja kumuona msanii huyo, ila kama meme zinavyotembea, WaTanzania walisema "Let me see you," Kizz Daniel akajibu, "wolololo"😂😂😂😂, make kwanza nicheke....

WaTanzania hao haoa ndio waliolipia bei za hadi sh150,000 kwa mmoja na zaidi ya sh milioni 10, ili tu kumuona msanii huyo afu akazingua.

Habari za kunyapianyapia ni kwamba mzee wa buga bwana aligomea kuperform toka akiwa Nigeria, akisingizia ndege, ila kamati ya maandalizi ikahakikisha kuwa anafika, baada ya hapo, bado kufika hotelini Dar, akadai kuwa amesahau begi lake la nguo Nigeria, hivyo hatoperform... wakahangaika wee kumpa nguo mpya ila wapii, kijana akajifungia hotelini, huku wananchi wenye hasira kali wakizidi kukosa raha ukumbini.

Hata hivyo, taarifa hizi bado tunazofuatilia, kwani kamati ya maandalizi (str8up vibes) wametoa tamko la kuomba msamaha na kuitisha press conference jioni hii.

Huku hayo yakiendelea, katika video zilizotifikia hivi punde, Kizz Daniel alionekana kufuatwa na polisi hotelini na kuchukuliwa kuelekea kituoni, ambapo kwenye  video hizo, alisikika mtu mwenye lafudhi ya kiNigeria akisema kuwa, "Umeona sasa, nilikubembeleza jana kwa masaa mawili, ona sasa."

Kwa habari zaidi, endelea kufuatilia Mwananchi Scoop.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags