Bongo Ni Tamu Atakaye Na Aje...

Bongo Ni Tamu Atakaye Na Aje...

Achana na Nonda Shaaban Papii. Aliyekuja na kupita njia kuelekea Ulaya. Wapo kina Ben Mwalala na Bonaface Ambani. Niyonzima, Mbuyu Twite, Kiiza, Mavugo, Amis Tambwe. Kavumbagu na Kahata. Waliigeuza Bongo kama kwao.

Hakukauka Tanzania kila msimu Emmanuel Okwi. Tukadhani ama anavutiwa na pisi na amani ya Bongo. Chirwa kalowea kabisa. Kagere kama mpiga kura wa Maneromango. Yes! Chama na Konde Boy walisepa wakarudi.

Muhuni kutoka Ghana Benard Morison. Beki hazikabi kabisa na Bongo. Aliomba uraia ili awe Mmatumbi kamili. Kunani Bongo? Mbona wageni wanagoma kurudi kwao? Zamani tulipokea wageni wa kisiasa, sasa ni wanasoka.

Utamaduni wa kusepa na kurudi umehamia kwa makocha sasa. Uchebe aliifikisha Simba robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Walimtema, akarudi kwa Singida Black Stars. Kaze alitua Yanga na kuondoka. Baadaye alijiunga na Namungo.

Gamondi alitimuliwa na Yanga, sasa karudi kwa Singida Black Stars. Marcio Maximo aliletwa na Jakaya kwa Taifa Stars. Akasepa baada ya miaka kadhaa akaletwa tena na Yanga. Wakamchoka nao wakamtimua.

Amarudi na KMC wanammiliki.
Bongo wanakuja na kuondoka kwa nini? Malisho mazuri? Ama wanakosa soko nje ya Bongo?
Wakati wageni wakija na kusepa zao. Wazawa wanawapokea bila wao kuondoka.

Chama aliondoka akarudi tena.
Mkude, Kapombe na Zimbwe Jr wa hapa hapa. Kisinda aliondoka akarudi na Mudathir akikutwa hapa hapa Bongo. Aziz Ki alikuja na kaondoka, Feitoto akiwa hapa hapa. Nina shaka Mayele atarudi amkute Mzize hapa.

Makocha wanakuja na kuondoka wenyeji wakiwa wasaidizi wao.
Mataifa jirani huleta makocha.
Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na Congo. Lakini
makocha wazawa wanafurahia tu kuwa wasaidizi wao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags