Unafahamu Maana Ya YKK Kwenye Zipu

Unafahamu Maana Ya YKK Kwenye Zipu

Umewahi kugundua kuwa zipu nyingi tunazotumia kwenye mikoba, nguo, na hata mabegi huwa zimeandikwa herufi YKK?

Leo fahamu maana ya herufi hizo. YKK ni kifupisho cha maneno ya Kijapani “Yoshida Kōgyō Kabushiki Kaisha” (吉田工業株式会社), ambayo kwa tafsiri ya Kiingereza ni 'Yoshida Manufacturing Corporation.

Ni jina la kampuni ya kutengeneza zipu iliyoanzishwa mwaka 1934 na Tadao Yoshida huko Tokyo, Japan. Yenye lengo la kutengeneza zipu zenye ubora wa hali ya juu lengo ambalo bado linaendelezwa hadi leo.



Hata hivyo wengi hujikuta wakitumia zipu zilizoandikwa YKK bila kufahamu maana yake. YKK ina viwanda zaidi ya 70 katika nchi zaidi ya 50 duniani, jambo ambalo linawezesha kuwahudumia wateja wake kwa haraka na kwa ufanisi. Leo hii, YKK inatengeneza sio tu zipu bali pia na bidhaa nyingine kama vile vifungo, sehemu za plastiki, na vifaa vya ujenzi.

Ikumbukwe YKK si kiwanda pekee duniani kinachozalisha zipu, lakini ndicho kikubwa zaidi na maarufu zaidi kwa sababu ya ubora wa bidhaa zake na usambazaji wa kimataifa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags