Wengine Wawili Waongezeka, Kesi Ya Diddy

Wengine Wawili Waongezeka, Kesi Ya Diddy

Waendesha mashitaka wa serikali ya Marekani wameripotiwa kuleta waathiriwa wengine wawili wanaodaiwa kuwa na madai mapya dhidi ya ‘Rapa’ Diddy.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Hollywood Unlocked’ mashitaka hayo yaliwasilishwa mapema jana Alhamis Januari 30, 2025 katika Mahakama jijini New York yanaeleza kuwa waasirika hao wawili ambao hawajawekwa wazi majina yao walihusishwa katika biashara za usafirishaji wa ngono huku mtuhumiwa akitumia nguvu na vitisho ili watu hao wakae kimya.

Aidha kwa mujibu wa mawakili wa Diddy wanaeleza kuwa mashitaka hayo mapya hayana ukweli wowote na Combs yupo tayari kupambana na yoyote mahakamani.

“Mashtaka mapya hayana makosa mapya. Nadharia ya upande wa mashtaka bado ina upungufu mkubwa, Serikali imeongeza nadharia ya kijinga kwamba wapenzi wawili wa zamani wa Bw. Combs hawakuwa wapenzi kabisa bali walikuwa makahaba. Kwa sasa mteja wetu amejikita zaidi kupambana na mashititaka hayo na kushinda kesi mahakamani,” amesema wakili wa Combs, Marc Agnifilo

Mpaka kufikia sasa Diddy anakabiliwa na kesi za unyanyasaji wa kingono takribani 15, alikamatwa kwa mara ya kwanza Septemba 16, 2024 jijini New York katika moja ya hoteli iliyopo jijini humo, akikabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa ngono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Mei 5, 2025. Kwa sasa rapa huyo amezuiliwa katika gereza la MDC Brooklyn.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags