Kisa Mzozo Rwanda Na Congo, Tems Aahirisha Show

Kisa Mzozo Rwanda Na Congo, Tems Aahirisha Show

Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria, Tems ametoa taarifa ya kughairisha tamasha lake alilopanga kulifanya nchini Rwanda kufuatia machafuko yanayoendelea katika nchi ya Congo na Rwanda.

Kupitia ukurasa wake wa X (zamani twitter) ameomba radhi kwa mashabiki kufuatia na kuendelea kufanya promo ya tamasha hilo bila kujua kuwa kuna mgogoro unaendelea kati ya nchi hizo mbili.

“Hivi majuzi nilipromoti tamasha langu Rwanda bila kujua kuwa kuna mgogoro unaoendelea kati ya Rwanda na Congo, Sikuwahi kamwe kuwa na nia ya kupuuza masuala halisi ya dunia, na ninaomba radhi kwa dhati ikiwa hili lilionekana hivyo.

Sikuwa na wazo lolote kwamba hili linaendelea. Moyo wangu uko kwa wale walioathirika. Migogoro si jambo la mzaha, na kwa kweli natumaini na kuomba amani katika kipindi hiki,” ameandika Tems huku akishare taarifa kuwa tamasha hilo halitofanyika.

Utakumbuka Tems alipanga kufanya show katika nchi hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya ‘Born in the Wild’ ambapo alipanga kukiwasha nchini humo Machi 22, 2025 katika ukumbi wa BK Arena.

Rwanda imetuhumiwa na Umoja wa Mataifa, serikali za Magharibi, na mamlaka za Congo kwa kuunga mkono kundi la waasi la M23, ambalo limehusika na kuongezeka kwa ghasia na ukimbizi katika mashariki mwa DRC.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags