Wema Sepetu afundwa na Bodi ya Filamu

Wema Sepetu afundwa na Bodi ya Filamu

Mwigizaji Wema Sepetu amesema kuitwa kwake na Bodi ya Filamu Tanzania kumemfanya atambue thamani yake.

Wema amesema hayo leo Mei 22,2025 baada ya kumaliza mazungumzo katika ofisi ya bodi hiyo ambapo aliitwa kutokana na vazi alilokuwa amevaa wiki iliyopita kudaiwa halina staha.

“Labda niseme kwamba mzungumzo baina yangu mimi na Bodi ya Filamu yalikuwa ni mazungumzo ya kirafiki sana, tulikuwa tunakumbushana kwa sababu hata mimi nilikuwa naogopa.

"Lakini hayakuwa yako vile nilivyokua nategemea ni katika kuwekana sawa. Pia nimejisikia vizuri kwa sababu nimetambua thamani yangu na nimeona ni jinsi gani ninavyopendwa kwa sababu ningekuwa nimeachwa tuu nisingeambiwa chochote wala kuitwa au kukanywa,”amesema

Aidha ameongezea wito huo umefanya aone anapendwa na kujaliwa na Bodi hiyo inayosimamia wasanii wa maigizo nchini

“Anayekukanya ni mtu ambaye anakupenda na anakujali ni mtu ambaye anakuona kwa ukubwa zaidi. Kwahiyo kile ambacho kimetokea hakikustahili kutokea kwangu na hicho ndio kitu ambacho tumekumbushana pia na viongozi wangu, nashukuru tumemaliza vizuri,” amesema Wema

Hata hivyo kwa upande wake Gervas Kasiga ambaye ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania amesema wamemuita Wema kumkumbusha maadili na thamani yake aliyojitengenezea katika tasnia ya maigizo nchini

"Tumemuita Wema ili kumkumbusha thamani yake na wajibu alionao katika jamii kama mwanatasnia aliyejitengenezea thamani katika tasnia, kwahiyo kuna haja pia na yeye kuiona thamani anayopewa na kuilinda kimaadili," amesema Gervas

Amesema hata kama mwigizaji huyo alikuwa amevaa vazi lile katika maisha yake binafsi ikiwa ni njee ya sanaa bado inamshushia thamani kama kioo cha jamii.

"Tunazungumzia wajibu wa msanii kuikomba jamii katika mambo mabaya, sasa msanii kama msanii una maisha yako binafsi lakini maisha yako binafsi yanabebwa na ile thamani kubwa ambayo umeijenga kwa hiyo mtu mwenye thamani kubwa akionekana amefanya jambo baya hata kama ni maisha yake binafsi inakuwa siyo jambo zuri," amesema Gervas.

Amesema licha ya muigizaji huyo kutambulika pia kama Miss Tanzania mwaka 2006 ambapo tasnia hiyo inaruhusu kuvaa mavazi tofauti tofauti kulingana na mazingira bado hakutakiwa kuvaa vile maana anatambulika kama msanii wa maigizo.

"Sisi kama Bodi ya Filamu tunafanya uzingatiaji wa maadili ya nchi kwa waigizaji na Wema ni moja ya watoto wetu ambaye anathamani kubwa katika uigizaji kwahiyo haikuwa sawa kuvaa vile" amesema Gervas






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags