Wakati mashahidi wakiendelea kuongezeka mahakamani kufuatia na kesi ya Diddy, na sasa imeripotiwa kuwa aliyekuwa mfanyakazi binafsi wa Diddy, George Kaplan, siku ya jana Jumatano Mei 21, 2025 alitoa ushahidi katika kesi hiyo huku akiweka wazi kuwa alitumika kuandaa vyumba kwa ajili ya matukio ya kingono.
Kaplan alieleza kuwa alifanyakazi kwa rapa huyo kuanzia mwaka 2013 hadi 2015, kwa mshahara wa dola 125,000 kwa mwaka huku akifanyakazi masaa 80 hadi 100 kwa wiki. Akiwa kazini hapo, anadai kuwa Diddy alikuwa akimtishia kumfukuza kazi kutokana na upole wake.
Aidha alieleza kuwa alitumika katika maandalizi ya vyumba vya Hoteli za kifahari kama InterContinental iliyopo Los Angeles na Trump International huko New York kuhakikisha anaandika jina la ‘Frank Black’ ambalo hulitumia Diddy kuingia kwenye hotel, kuandaa mabegi yaliyojaa vitu vyote vya msingi kwa ajili ya ngono kama mishumaa, mafuta lainishi ya Astroglide, mafuta ya watoto ya Johnson & Johnson, na vinginevyo, na kisha kuyapanga ndani ya vyumba vya hoteli.
Vile vile alitumika kusafisha vyumba vya hoteli baada ya matukio hayo ya kingono kukamilika huku akidai kuwa alitumika kusafisha kwa lengo la kulinda jina la Diddy na siri zinazofanyika zisionekane na wafanyausafi wa hoteli hizo. Alikusanya chupa za mafuta ya watoto, pombe, na vinywaji vya Gatorade, na mara moja alipata “poda ya kahawia iliyoganda” juu ya sinki la bafuni.
Mbali na hayo lakini pia Kaplan aliweka wazi kuwa wakati mwingine alitumwa kununua dawa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na MDMA, ketamine, na Advil na kwenda kuziweka katika hoteli.
Mpaka kufikia sasa zaidi ya mashahidi watano wameshatoa ushahidi kesi dhidi ya Diddy akiwemo aliyekuwa mpenzi wa rapa huyo Cassie Ventura, Mama wa Cassie Ventura, Dr. Dawn Hughes, Gerard Gannon. Huku msanii Kid Cudi akitarajiwa kutoa ushahidi kuhusu vitisho alivyopokea kutoka kwa Diddy baada ya kugundua uhusiano wake na Cassie.
Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York, baada ya kufunguliwa mashtaka ya shirikisho yanayohusisha njama ya kihalifu (RICO), usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono kwa nguvu, udanganyifu au kulazimisha, na kusafirisha watu kwa ajili ya biashara ya ngono.
Kabla ya kukamatwa kwake nyumba za msanii huyo nyumba zake zilifanyiwa upekuzi na maafisa wa Idara ya Usalama wa Ndani (Homeland Security Investigations - HSI) Machi 25, 2024. Upekuzi huo ulifanyika katika nyumba zake mbili ya Holmby Hills huko Los Angeles na ya Star Island huko Miami Beach.
Katika upekuzi huo vilipatikana vitu mbalimbali ikiwemo bunduki aina ya aina ya AR-15, midoli ya ngono, viatu virefu vya kisigino (stilettos), vifaa vya BDSM, na zaidi ya chupa 1000 za mafuta ya watoto na vilainishi, madawa ya kulevya na vinginevyo.
Mpaka kufikia sasa msanii huyo amekana mashitaka yote na endapo atakutwa na hatia atakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

Leave a Reply