Chris Brown Aachiwa Kwa Dhamana

Chris Brown Aachiwa Kwa Dhamana

Nyota wa R&B kutoka Marekani Chris Brown, ameachiwa kwa dhamana na mahakama Jijini London leo Jumatano Mei 21, 2025, baada ya kukaa rumande kwa takribani siku sita.

Chris ameachiliwa baada ya kuahidi kulipa dhamana ya dola 6.7 milion sawa na Sh17.42 bilioni kama fidia kwa mtayarisha wa muziki nchini humo anaefahamika kama Abraham Diaw.

Inaelezwa kuwa Brown hakuwepo mahakamani hapo wakati dhamana yake inatolewa, lakini ametakiwa kuwasilisha Passport yake itakayoshikiliwa na mawakili na polisi wakati atakapotaka kusafiri kwenda nchi nyingine kwa ajili ya kazi zake.

Hatahivyo, Kesi yake imepangwa kusikilizwa tena Juni 20, 2025, katika Mahakama hiyo, Lakini Breezy ameruhusiwa kuendelea na ziara yake ya kimataifa ya muziki, ambayo inajumuisha maonesho kadhaa nchini Uingereza, Marekani na Canada mwezi Juni na Julai.

Chris Brown alikatamatwa Alhamis ya Mei 15, 2025, alipotua na ndege binafsi nchini Uingereza ambapo amesota ndani kwa siku sita hadi kuachiliwa leo kwa dhamana hiyo.

Brown alishitakiwa na Abraham Diaw baada ya kumshambulia bila sababu wakati nyota huyo na wapambe wake wakiwa kwenye klabu ya usiku ya Tape nchini humo mwaka 2023.

Akizungumza na gazeti la The Sun mtayarishaji huyo alisema Breezy alimpiga na chupa ya mvinyo mara mbili kichwani na kwenye goti.

"Alinipiga kichwani mara mbili au tatu. Goti langu lilianguka pia." amesema Diaw.

Inaripotiwa kuwa baada ya tukio hilo mtayarishaji huyo alizimia na kupelekwa hospitalini na alihitaji magongo ya kutembelea hata baada ya kuruhusiwa.

Utakumbuka mtayarishaji huyo alifungua madai dhidi ya Brown huku akitaka kulipwa dola milioni 16 sawa na Sh43 bilioni kama fidia ya majeraha na hasara iliyopatikana kutokana na shambulio hilo.

Kuachiliwa kwa Chris Brown kunakuja ikiwa zimesalia wiki kadhaa kabla ya mwimbaji huyo kuzindua ziara yake ya ulimwengu ya Breezy Bowl XX, ambapo amepanga kutumbuiza Uingereza kwa siku mbili mfurulizo Juni 21 na 22, 2025 katika Uwanja wa Tottenham Hotspur wa London.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags