Bieber: Kumuoa Hailey Ulikuwa Uamuzi Bora Kwangu

Bieber: Kumuoa Hailey Ulikuwa Uamuzi Bora Kwangu

"Nimefanya mambo mengi ya kijinga maishani mwangu, lakini kumuoa Hailey ndio jambo la akili zaidi nimewahi kufanya". Hii ni kauli ya mwanamuziki Justin Bieber akiliambia jarida kubwa duniani la 'Vogue' wakati akifanya mahojiano na mwandishi Rhode.

Msanii huyo ambae hivi karibuni amekuwa akiripotiwa kupitia changamoto ya afya ya akili na ukosoaji mwingi kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kubadalika kwa mtindo wake wa maisha, kupitia chapisho la Vogue lililotoka Jumanne, Mei 20, 2025, linalohusu wasifu wa Bieber, Hailey Bieber msanii huyo alisema.

“Nimefanya mambo mengi ya kipumbavu maishani mwangu, lakini jambo la busara zaidi ambalo nimewahi kufanya ni kumuoa Hailey,”alisema Bieber.

Hata hivyo msanii huyo katika mahojiano yake ameonekana kufurahia uwepo wa mke wake kama ubavu wa kuegeme katika kipindi kigumu anachokipitia kufuatia na ukosoaji anaoupata wa mwonekano wake huku baadhi ya mijadala ikidai kuwa Bieber amekuwa katika hali hiyo kufuatia na kushuka kiuchumi.

Bieber na Hailey walifunga ndoa ya kiserikali mwaka 2018 na baadae kufanya sherehe ya harusi iliyojaa mastaa mbalimbali mwaka 2019. Huku Agosti 23, 2024 wawili hao walitangaza kupata mtoto wao wa kwanza wakiume aitwaye Jack Blues Bieber.

Katika makala hiyo ya Vogue inayoelezea wasifu wa Hailey, mwanadada huyo amesema kwa upande wake amekuwa akikutana na ukosoaji kumuhusu licha ya mume wake Justin kumpambania ili watu wamuelewe.

"Amepigana sana kujaribu kuwafanya watu wanielewe, au kujua mimi ni nani, au kuniona kwa ajili yangu lakini watu hawataki.

Baada ya kuzaa ndio wakati mbaya zaidi ambao nimewahi kupitia maishani mwangu, na kujifunza mimi mpya mwenyewe ni ngumu sana, wakati wote kwenye mitandao kila siku watu huwa wanasambaza taarifa kuwa 'Wanaachana' na 'Wako hivi' na 'Hawana furaha, Siwezi hata kuanza kuelezea. Ni maisha ya kichaa kuishi" amesema Hailey.

Anamesema amejifunza kutoka kwa mume wake Justin, uvumilivu wa kukabiliana na maneno ya chuki kutoka kwenye maoni ya watu katika mitandao ya kijamii.

”Nimejifunza mengi kutoka kwa Justin kwa kweli, mekuwa akifanyiwa hivi tangu akiwa mtoto na imebidi akabiliane na uchunguzi zaidi wa mtu yeyote ninayemjua,” amesema Hailey.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags