Vitu Vilivyopatikana Kwenye Chumba Cha Diddy Vyaanikwa

Vitu Vilivyopatikana Kwenye Chumba Cha Diddy Vyaanikwa

Maafisa usalama wa serikali kuu nchini Marekani wametoa ushahidi mahakamani kwamba walikuta dawa za kulevya, mafuta ya watoto, vilainishi na kiasi kikubwa cha pesa taslimu zilizokuwa zimefichwa kwenye chumba cha Sean Diddy Combs katika Hoteli ya Park Hyatt New York City, Marekani.

Picha hizo kutoka katika chumba cha Diddy katika hoteli hiyo zimewasilishwa mahakamani kama ushahidi wa kesi zinazomkabili rapa huyo.
Kulingana na nyaraka mpya za kisheria zilizo patikana na TMZ maafisa wa serikali walikamata mifuko miwili ambapo ndani ya mifuko hiyo kulikuwa na vitu vyenye rangi ya waridi maabara imethibitisha kuwa mfuko mmoja ulikuwa na dawa za katamine na mwingine ulikuwa na mchanganyiko wa MDMA na Ketamine, mifuko hiyo ya dawa imeoneshwa mahakamani wakati wa ushahidi kwa kila mjumbe wa baraza la majaji ili wajionee kwa ukaribu.



Kwa mujibu wa Mamlaka ya kupinga Dawa za Kulevya Marekani, Ketamine ni dawa inayoathiri uwezo wa kuona na kutoa sauti ambapo humfanya mtumiaji kujihisi mchovu na kushindwa kujidhibiti na MDMA hufanya kazi kama kichocheo na hutoa athari ya kuchangamsha, hupotosha wakati na mtazamo kwa mtumiaji.

Aidha, maafisa hao wametoa ushahidi kuwa dawa aina ya Clonazepam ilipatikana ndani ya chupa ya dawa yenye jina la Frank Black ambapo mpenzi wa zamani wa rapa huyo Cassie Ventura alithibitisha kuwa Frank Black ni jina la bandia ambalo Diddy amekuwa akilitumia.

Wakala Maalumu aliyepiga picha za ushahidi huo, Yasin Binda ameeleza kuwa katika moja ya begi lilopatikana kwenye kabati la chumba cha Diddy hotelini hapo, kulikuwa na mfuko wa Ziploc uliyojaa mafuta ya watoto 'Baby Johnson' na mwingine ukiwa umejaa mafuta ya vilainishi 'Astroglide'

Hata hivyo, katika muendelezo wa taarifa nyingine kumhusu rapa huyo ni kuwa wafanyakazi wa ngono wanaodaiwa kuhusishwa naye katika vitendo vya ngono wamefichuliwa rasmi. Siku ya Jumatatu Mei 19, 2025, waendesha mashtaka wa serikali walitoa nyaraka mpya mahakamani ikiwa ni pamoja na picha na taarifa za kina kuhusu mtandao wa wafanyakazi wa ngono wa rapa huyo.



Kwa mujibu wa ushahidi wa serikali inadaiwa kuwa Diddy aliwalazimisha kushiriki katika matukio hayo ya ngono na kuwarekodi mwenyewe, picha zilizooneshwa mahakamani zinaonesha sura za wafanyakazi hao huku kila mjumbe wa baraza la majaji akipewa nafasi ya kuwatazama kwenye skrini yake.

Cassie aliyekuwa mpenzi wa Diddy na shahidi muhimu kwenye kesi hiyo aliwatambua baadhi yao ingawa hakukumbuka majina ya wengine, wanaume waliyotajwa ni pamoja na Jonathan Old Jay kutoka Los Angeles, Craig kutoka Miami, Brian kutoka New York na wengine wengi.
Kesi dhidi ya Diddy inaendelea kusikilizwa huku ushahidi ukiendelea kutolewa mahakamani hapo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags