The Weeknd Awapiga Chini Drake Na Justin Bieber

The Weeknd Awapiga Chini Drake Na Justin Bieber

Mwanamuziki kutoka Canada, The Weeknd ameendelea kuonesha ukubwa wake kwenye muziki ambapo ametangazwa kuwa msanii maarufu zaidi Canada akiwapiku mastaa wakongwe wenye ushawishi mkubwa kama Drake na Justin Bieber.

Takwimu mpya kutoka mitandao kama Spotify na Apple Music imeonesha kuwa The Weeknd ndiye msanii wa Canada mwenye wasikilizaji wengi zaidi, akiwa na streams zaidi ya bilioni 13 kwa mwaka mmoja huku akiongoza kwa kuwa na nyimbo maarufu ikiwemo ‘Blinding Lights’.

Mbali na hayo mwaka 2023 kwa mujibu wa ripoti ya Guinness World Records, The Weeknd alifikisha rekodi ya kuwa msanii wa kwanza duniani kufikisha wasikilizaji milioni 100 kwa mwezi mmoja kwenye mtandao wa Spotify hatua ambayo haijafikiwa na Drake wala Justin Bieber.

Aidha msanii huyo pia miezi michahce iliyopitwa alitangazwa kuwa mmoja wa wasanii walioingiza pesa ndefu kupitia ziara zao ambapo kupitia ziara yake ya Aftrer Hours Till Dawan’ alifanikiwa kuingiza dola 350 milioni ikiwa ni zaidi ya Sh943.2 bilioni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags