Mfahamu Rayyan Arkan Mtoto Anayetamba Mitandaoni

Mfahamu Rayyan Arkan Mtoto Anayetamba Mitandaoni

Rayyan Arkan Dikha, mtoto mwenye umri wa miaka 11 kutoka Indonesia, kwa sasa amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii duniani kote baada ya video yake akiwa nadansi ikiwakosha wengi.

Kupitia video hiyo Rayyan anaonekana akicheza kwa ustadi mkubwa mbele ya mashua ya kasi wakati wa tamasha la kitamaduni la Pacu Jalur, huku akionyesha miondoko ya kipekee iliyowavutia wengi na kuifanya staili yake kupendwa na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa soka kama Travis Kelce na Alex Albon.



Rayyan alizaliwa Desemba 28, 2014, katika mji wa Kuantan Singingi, mkoani Riau, Indonesia. Kwa sasa ni mwanafunzi wa darasa la tano, na alianza kucheza juu ya mashua akiwa na umri wa miaka 9. Inaelezwa kuwa kipaji chake hicho hakijatokana na madarasa ya dansi bali alijifunza kutoka kwa baba yake na mjomba wake ambao ni wanariadha wa mashindano ya Pacu Jalur.

Katika mahojiano yake na BBC, Rayyan alifichua kuwa miondoko yake ya dansi haikupangwa bali ilimjia tuu kichwani ghafra. “Nilibuni mwenyewe pale pale. Ilikuwa ni ghafla tu. Kila mara marafiki zangu wanapokuona wanasema ‘umetrend mtandaoni,”amesema Rayyan.

Umaarufu wake umezaa matunda kwake na kwafimilia yake ambapo aliteuliwa kuwa balozi wa utamaduni na Gavana wa Riau, na pia alipata nafasi ya kukutana na mawaziri wa utamaduni na utalii huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia. Lakini pia alionekana kwenye televisheni ya taifa akitumbuiza pamoja na mama yake mzazi.

Aidha Waziri wa Utamaduni wa Indonesia, Fadli Zon, alisema kuwa kucheza juu ya mashua ya kasi si kazi rahisi, kwani inahitaji mizani na ujasiri, jambo ambalo watoto wanaweza kulimudu vyema kuliko watu wazima, huku Mama yake Rayyan, Rani Ridawati, alikiri kuwa aliwahi kuwa na hofu mwanawe anaweza kudondoka na kuumia lakini kwasasa hana hofu tena kutokana na kuwepo na kikosi kizuri cha uokoaji.

Mbali na hayo wakati wa mahojiano yake Rayyan ameweka wazi kuwa ndoto yake kubwa ni kuwa askari polisi ili kuweza kuitumikia jamii yake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags