Mwanamuziki Nandy ameweka wazi changamoto anazokumbuna nazo kwenye ndoa akieleza kuwa ni mumewe kuchanganya muda wa familia na marafiki.
“Ilikuwa changamoto kubwa mwanzoni ni kuchangaja muda wa marafiki na familia hiyo ilikuwa changamoto yangu kubwa, namshukuru Mungu jinsi nilivyoendelea kukuaa ameelewa moyo wangu unataka nini kwake.
Ndoa ni nzuri mkiwa mnaelewana unaweza ukamwambia mtu ndoa iko hivi na hivi lakini ndoa hazifanani kwa sababu pia binadamu hawafanani binadamu wangu huyu niliyopewa tofauti na mwingine atakayepewa lakini kwangu mimi changamoto ni hizo za kawaida na hatujafikia changamoto kubwa unasema hapa ndoa inaweza kuyumba, anajaribu kila siku kuwa bora kwa ajili yangu,”amesema Nandy
Nandy ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahijoano na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo Julai 17,2025 katika sherehe ya kumbukizi ya ndoa yao ambayo imetimiza miaka mitatu sasa tangu wafunge ndoa mwaka 2022.
Aidha kwa upande wa mume wake Billnass ameweka wazi kuwa tangu afunge ndoa na mke wake Nandy miaka mitatu iliyopita hajawahi kuchepuka.
“Kuna muda nikikaa nampongeza sana mke wangu kwa kunivumilia mtu kama mimi najijua ni mwanadamu sijakamilika kuna vitu kukosea na mimi sijawahi kuchepuka na sifikirii kufanya jambo la namna hiyo,”amesema Billnass
Leave a Reply