Mchekeshaji Hassan Kazoa ‘Mr Food’ameweka wazi ugumu anaopata katika kunakilisha sauti ‘Dubbing’ kama mlemavu.
Akizungumza na Mwananchi Kazoa, ambaye anaingiza sauti ya mlemavu aitwaye Basil kupitia tamthilia ya ‘Crystal’ inayooneshwa katika kisimbuzi cha Azam Tv ameeleza kuwa ugumu anaopata ni sauti kukauka.
“Ugumu ninaopata kwanza ni kuvaa uhusika wa mtu kama yule, nadhani wote mnamuona hayupo sawa kiakili na kimwili. Kwa hiyo je unaaminishaje watu kwamba kweli huyu mtu anatatizo. Yaani sauti yangu iendane na uhalisia wake wa ulemavu wa mwili pamoja na mdomo, napata ugumu sana nikiwa ndani ya studio nakuwa natumia nguvu.
“Muda mwingine sauti inakuwa inaleta shida. Pia kuna muda natakiwa kupindisha mdomo ili kupata test yenyewe ya yule anavyoongea. Kwa hiyo naweza kusema ugumu upo jasho lazima litoke. Niseme ukweli tu kazi ya kunakilisha sauti ni kazi ngumu watu wasione vile kwenye Tv lakini ni ngumu sana na ili kazi iende vizuri lazima uwe na chembechembe za sanaa,” amesema Kazoa
Akizungumzia kuhusu ulaji wake namna anavyokata matonge makubwa, ambapo ameeleza kwake ile ni sanaa na huwa anafanya mazoezi na ndio maana haimpi shida anapokuwa mbele ya kamera.
“Haiwezi kunipa shida kwa sababu ni moja ya kazi yangu na kabla ya kula matonge makubwa kama ambavyo watu wanaona kwenye baadhi ya clip zangu huwa nafanya mazoezi makubwa. Yale matonge sio kama nakurupuka tuu hapana huwa nafanya mazoezi ya vitendo pia.
“Nafanya mazoezi kila siku na ndio maana napata idea mpya mfano kunatonge la kuswipe, kufuta kuna tonge lile kama kichwa cha mtoto yote hayo ni kwa sababu ya mazoezi. Nyumbani siwezi kula vile kwanza mimi sio mlaji nikiwa nyumbani nakula kawaidia tuu, watu wasitishike nikiwa mbele ya kamera nitofauti na nikiwa nyumbani,”amemalizai Kazoa
Mbali na hayo kuhusu kutamani kuingia kwenye tamthilia na filamu amewaomba waongozaji na waandishi wamtazame kwa jicho la tatu kwani anaamini anakipaji.
“Natamani kuingia kwenye tamthilia kwa sababu ni moja ya ndoto na kipaji changu. Siwezi kulaumu sana kwa sababu labda waongozaji hawajaona nafasi yangu kuwepo kwenye tamthilia.
“Natamani na naomba watazame kipaji changu mara mbili mbili, niwaambie tu milango iko wazi sina kipingamizi chochote ni makubaliano tu,” amesmea Kazoa

Leave a Reply