Tyler Perry Azikosoa Kampuni Za Bima, Janga La Moto

Tyler Perry Azikosoa Kampuni Za Bima, Janga La Moto

Mwigizaji Tyler Perry amezikosoa kampuni za bima kwa kutotumia njia bora za kusaidia jamii zilizoathiriwa na moto mkali unaoendelea jijini Los Angeles.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mwigizaji huyo amekerwa na uamuzi wa kufuta bima za baadhi ya wakazi wanaoishi katika maeneo ambayo yameathirika na moto.

“Kumtazama binti akitumia bomba la maji ya bustani kujaribu kulinda nyumba ya wazazi wake wa miaka 90 kwa sababu bima yao ilifutwa, kuliumiza moyo wangu, Je kuna mtu mwingine anayeona ni jambo la kusikitisha kwamba kampuni za bima zinaweza kuchukua mabilioni ya dola kutoka kwa jamii kwa miaka mingi, kisha ghafla, kuruhusiwa kufuta mamilioni ya sera za watu waliowafanya kuwa matajiri?.

Nikiwa katika mchakato wa kutafuta hatua za kuchukua ili kufanya kadiri niwezavyo kuwasaidia wengi kadri niwezavyo, ninawaweka wote kwenye maombi yangu,” ameandika Tyler Perry

Aidha kulingana na CBS News, inakadiriwa kuwa sera za bima 1,600 zilifutwa na ‘State Farm’ Julai 2024 katika eneo la Pacific Palisades, ambako moto ulisababisha uharibifu usio wa kawaida. Zaidi ya hayo, State Farm pia ilifuta zaidi ya sera 2,000 katika maeneo mawili mengine ya Los Angeles, yakiwemo mitaa ya Brentwood, Calabasas, Hidden Hills, na Monte Nido.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags