Kocha Guardiola Aachana Na Mke Wake

Kocha Guardiola Aachana Na Mke Wake

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameachana na mke wake Cristina Serra ambaye wamekaa pamoja kwa miaka 30.

Guardiola ambaye anapitia kipindi kigumu kwenye kikosi cha Manchester City alifunga ndoa na mke wake nchini Hispania mwaka 2014, wakiwa wameshakaa pamoja kwa muda mrefu, lakini jana iliripotiwa kuwa wameachana rasmi.

Taarifa ya kuachana kwao ilianza kutolewa na gazeti la Hispania Spanish Sport, likieleza kuwa wawili hao hawapo pamoja kwa miaka mitano tangu Serra alipoamua kuondoka England na kutimkia nchini Hispania akiwa na mtoto wake mmoja Valentina, 17, huku akimuacha Pep Manchester England akiwa na City.

Wawili ambao walikutana rasmi mwaka 1994 wana watoto watatu, Maria, 24, Marius, 22 na Valentina.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa awali hakukuripotiwa taarifa yoyote ya kutofautiana kwa wawili hao kwani pamoja na kuishi nchi mbili tofauti bado mara kwa mara walikuwa wanaonekana pamoja nchini Hispania na England kwa vipindi tofauti.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags