Waandaji wa tuzo za BET wametoa orodha ya wasanii wanaowania tuzo hizo huku Tanzania ikiwakilishwa na msanii pekee wa Bongo Fleva, Abigail Chams.
Abigail Chams amechaguliwa kuwania kipengele cha 'Best New International Act' ambapo atachuana na Ajuliacosta (Brazil), Amabbi (Brazil), Dlala Thukzin (Afrika Kusini), Dr Yaro (Ufaransa), KWN (UK), Maglera Doe Boy (Afrika Kusini), Merveille (Ufaransa), Odeal (Uk), Shallipopi (Nigeria), TxC (Afrika Kusini).
Wasanii wa Kiafrika wengine waliotokea katika orodha ya kuwania tuzo hizo ni Rema (Nigeria), Ayra Starr (Nigeria), Tyla (Afrika Kusini), Black Sherif (Ghana) ambao wanawania kipengele cha Best International Act. Pia, Burna Boy anawania kipengele cha Msanii Bora wa Hip Hop ambapo anachuana na BigXthaPlug, Bossman DLow, Drake, Future, Kendrick Lamar, Key Glock, Lil Wayne, na Tyler The Creator.
Katika tuzo hizo msanii ambaye anawania vipengele vingi zaidi ni rapa kutokea nchini Marekani, Kendrick Lamar ambaye anawania vipengele 10 ambavyo ni pamoja na Msanii Bora wa Hiphop wa Kiume, Albamu Bora ya Mwaka, Video Bora ya Mwaka 'Not Like Us', Wimbo Bora Wa kushirikiana '30 For 30' SZA Ft Kendrick Lamar na vingine vingi.
Kutoka Afrika msanii anayewania vipengele vingi katika tuzo hizo ni Ayra Starr (Nigeria) ambae anawania vipengele vitatu ambavyo ni Msanii Bora wa R&B na Pop, Msanii Bora Chipukizi, na Best International Act.
Wasanii wengine ambao wametokea kwenye kuwania vipengele vingi ni pamoja na Doechii, Drake, Future na GloRilla ambao wote wanawania vipengele sita kila mmoja.

Leave a Reply