The Weeknd, Kushtua Kiwanda Cha Muziki

The Weeknd, Kushtua Kiwanda Cha Muziki

Msanii The Weeknd ameweka wazi huenda albamu yake aliyopanga kuitoa januari 31, 2025 'Hurry Up Tomorrow' ikawa kazi yake ya mwisho kwenye muziki chini ya jina lake maarufu ambalo limemfanya kuwa staa mkubwa duniani.

Kwenye mahojiano aliyofanya mapema wiki hii na Jarida la Variety, The Weeknd ameelezea kuchoka na shinikizo la umaarufu na ushindani usiokoma.

"Ni hali ya akili ambayo sijaweza kuingia tena, sina hamu nayo tena, maisha ya umaarufu yanahitaji zaidi ya tuzo, mafanikio, na umashuhuri, na mchakato wake hauishi hadi mtu mwenyewe aweke kikomo" amesema The Weekend.

The Weekend anaonekana kukubali kuwa yupo kwenye nafasi nzuri ya kimuziki kwa wakati huu na kuishi msemo usemao Mtumbuizaji mzuri ni yule anaejua muda sahihi wakuondoka jukwaani.

"Ni lini muda mzuri wa kuondoka, kama si wakati wa kilele chako?" amesema The Weekend.

Utakumbuka nisiku chache Tangu Billboard kutangaza wasanii 100 bora waliofanya vizuri karne ya 21 huku msanii huyo akitokea kwenye nafasi ya 6 lakini pia wimbo wake wa Blinding Light ukiongoza kwenye orodha ya chati hiyo ya nyimbo 100 bora ambazo zimefanya vizuri kwa karne ya 21 yaani kuanzia miaka ya 2000 mpaka sasa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags