Msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux ametangaza kufanya harusi ya kitamaduni na mke wake Priscilla Aprili 17, 2025.
Jux ambaye alifunga ndoa na mke wake Priscilla Februari 7, 2025 Mbezi Beach Dar es Salaam, ametangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kushare video hiyo iliyosindikizwa na maneno ya kimahaba pamoja na tarehe husika ya tukio hilo ambalo litafanyika nchini Nigeria kwao na Priscilla.
Harusi hiyo itakuwa ya kitamaduni ikiwa ni mfululizo wa zile sherehe za baada ya ndoa yao ambazo alitangaza kuzifanya mwaka huu Nigeria na Tanzania.
Baada ya harusi hiyo ya kitamaduni Jux na mkewake wanatarajia kufanya tafrija nyingie Mei mwaka huu nchini ambapo itahusisha ndugu, jamaa, Marafiki, mashabiki na watu wengine wa karibu.
Hata hivyo, Jux na mke wake wamekuwa Nigeria tangu Machi, ambapo walihudhuria uzinduzi wa filamu ya Labake Olododo ambayo imechezwa na mama mzazi wa priscilla, Iyoboojofespris.

Leave a Reply