Grammy Yahairishwa Kufuatia Na Janga La Moto

Grammy Yahairishwa Kufuatia Na Janga La Moto

Kampuni inayoongoza kwa usambazaji wa biashara ya muziki duniani 'Universal Music Group' imetangaza kuahirisha baadhi ya matukio yaliyopangwa kufanyika usiku wa tuzo za Grammy mwaka huu kufuatia moto mkubwa Jijini Los Angeles.

Universal Music Group (UMG) ilitangaza kuhairisha badhi ya hafla ikiwa ni pamoja na onyesho la wasanii, na sherehe iliyopangwa kufanywa baada ya ugawaji wa tuzo hizo na badala yake itaelekeza pesa ambazo zingetumika kwenye hafla hizo na kusaidia walio athiriwa na janga la moto huko Los Angeles.

Hata hivyo, ukiachana na UMG Mastaa mbalimbali duniani wameonesha kuguswa na janga la moto unaoendelea huko Los Angeles akiwemo Beyonce ambae amechangia kiasi cha dola 2.5milioni sawa na Shillingi 6.2billioni, lakini pia The Weekend ambae ametangaza kuahirisha kutoa baadhi ya kazi zake ikiwemo album yake ya 'Hurry Up Tomorrow' ambayo amesogeza mbele hadi januari 31, 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags