Ngoma ambayo imembeba mwanamuziki kutoka Marekani Kendrick Lamar mwaka 2024 ya ‘Not like Us’ imetajwa kufikisha wasikilizaji bilioni 1.
Mtandao wa Spotify umetangaza kuwa wimbo huo ambao ulikwa ni dongo kwenda kwa Drake umefikisha wasikilizaji bilioni 1 katika Spotify ndani ya siku 249.
Mbali na wimbo huo kupata mafanikio hayo lakini pia ‘Not like Us’ ilimfanya msanii huyo kutajwa kuwa msanii bora wa mwaka 2024 kwenye mtandao wa kuuza na kusikiliza muziki wa ‘Apple Music
Utakumbuka kuwa Mei, 2024 Lamar aliachia wimbo huo kama dongo kwa Drake na kuwafanya wawili hao kuwanza kutoleana siri na maneno kupitia nyimbo.
Ikumbukwe kuwa bifu la Drake na Lamar lilianza baada ya Lamar kutoa ngoma iitwayo ‘Like That’ akijitambulisha kuwa yeye ni bora kuliko Drake huku akidai kuwa amewazika mastaa wote wanaomuunga mkono Drake kupitia albumu yake ya ‘For All The Dog’.
Leave a Reply