Kim Kardashian Kutoa Nguo Kwa Waathirika Wa Moto

Kim Kardashian Kutoa Nguo Kwa Waathirika Wa Moto

Mfanyabiashara na mmiliki wa kampuni ya mavazi ya SKIMS, Kim Kardashian ametangaza kutoa msada wa mavazi na vitu vingine kwa familia zilizoathiriwa na moto katika Milima ya Hollywood.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mfanyabiashara huyo ameshare taarifa kuwa kupitia kampuni yake ya SKIMS atachangia mavazi ili viweze kuwasaidia watu ambao wameathirika na janga hilo.

“Tumetoa msaada kwa Los Angeles Fire Department Foundation kwa ajili ya kutoa rasilimali muhimu kwa waokoaji wa kwanza mashujaa wanaolinda jiji letu. Zaidi ya hayo, tunatoa mchango mkubwa wa nguo za ndani, mavazi, na soksi kwa Baby2Baby ili kuwasaidia wale waliopoteza makazi yao kutokana na moto huu,” ameandika Kim

Aidha kwa mujibu wa tovuti ya Page Six imeripoti kuwa msaada huo umetolewa baada ya Kim kukosolewa na jamii kuhusiana na kutangaza mauzo aliyopyapata kwenye SKIMS katika kipindi cha janga hilo.

Mbali na hilo lakini pia familia ya Kim imeripotiwa kukimbia makazi yao yaliyopo Calabasas na Hidden Hill, Los Angeles kufuatia na moto huo ulioteketeza makazi pamoja na kuondao uhai wa baadhi ya raia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags