Moto Wamfanya Jennifer Lopez Amfikirie Ex Wake

Moto Wamfanya Jennifer Lopez Amfikirie Ex Wake

Mwigizaji na mwanamuziki Jennifer Lopez amedaiwa kuwa na wasiwasi na mashaka kuhusiana na aliyekuwa mume wake Ben Affleck baada ya kuondolewa kwenye nyumba yake iliyopo Pacific Palisades sehemu ambayo moto unaendelea kuwaka.

Chanzo cha karibu cha mwanadada huyo kiliiambia tovuti ya Page Six kuwa Lopez amekuwa na wasiwasi kuhusu hali ya afya Ben tangu alivyosikia amehamishwa.

Lopez, mwenye umri wa miaka 55, amedaiwa kumfuatilia Ben wakati wote huku akimueleza kuwa yupo kwa ajili yake na watoto wake ambao ni Violet (18), Seraphina (15) na Samuel (12) hivyo endapo atahitaji msaada yupo kwa ajili yake.

Licha ya Ben kuhamishwa katika makazi yake taarifa zinaeleza kuwa nyumba yake ipo salama kwani haijaathirika na moto huo hata kidogo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags