Msomi acha uzembe  zifuate fursa

Msomi acha uzembe zifuate fursa

Na Michael Anderson

 Zifuate nafasi za kufanikiwa zilipo, usikae ukisubiri zikufuate kama kilimo cha vitunguu ni mbeya, wewe Dar hapakufai nenda uone mambo yanaendaje. Kama dili za madini ziko Arusha nenda fuata yalipo. Mafanikio hayakutafuti fanya kila lengo kufikia ndoto zako.

ZINGATIA HAYA KUZIFIKIA FURSA

  1. Usiweke mayai yako yote kwenye kapu moja

Pambana huku na kule uko chuo unasoma sawa lakini usiache kufanya biashara usiache kujitolea tafuta watu waliopo kwenye mifumo wakupe fursa usitoke darasani ukafikia kupunzika tuu room fursa haitakufata huko ndani

  1. Ziba masikio

Ukisikiliza sana maneno ya watu hautafanya lolote kwenye maisha mara fulani yuko hivi mara yuko vile sio ishu sana. Wewe muamini Mungu wako na fanya yako watu wataongea tu hata kama unafanya mazuri au mabaya so focus on your things.

  1. Kuwa na mshauri zumri anayekuongoza

Marafiki zako chuoni ndugu zako mjomba, baba, mama au hata mtumishi mwenzako ambaye atakuwa na experience zaidi ya maisha. Hawa watu wameona mbali lakini wamekutana na vitu vingi kabla yako na kama wako wazi katika mioyo yao basi watakupa walau mwanga wa jinsi ya kujipanga na baadhi ya mambo. Ukichukua mawazo yao ukachanganya na yako mambo yatakuwa safi.

USIFANYE HAYA UTAZIKOSA FURSA

  1. Kufanya kuwapendezesha wengine

Unafanya maamuzi kwa sababu ya kuwapendezesha mengine, unanunua vitu vya gharama kuwapendeza wengine, unaishi maisha nje ya kipato chako hivi utashindwa kufika kwenye malengo yako na fursa zilizopo mbele yako kwa kupendezesha wengine utakosa fursa

  1. Acha priviledge chukua majukumu

Acha kuwa unapenda upendeleo chukua wajibu usikose fursa usiingie sehemu wanapokufahamu ukaanza kuweka ukaribu kwa sababu unaamini kuna priviledge fulani utaipata. Chukua wajibu kufikia ndoto zako mapema na utapoteza fursa nyingi kwa sababu unapoteza trust.

  1. Kupoteza muda

Watu wengi hawajui kwamba muda uliokua nao sasa hivi hauwezi kurudi tena. Kijana msomi wa chuo muda wote anaangalia movie, kuchati wasiliana na watu ambao wapo kwenye cycle yako usipoteze muda kwenye vitu ambavyo havikupi fursa

  1. Kushindwa kujifunza ujuzi fulani

Mafanikio yako yamefichwa kwenye ujuzi maalumu. Chagua ujuzi mmoja mpaka tatu katika aina za ujuzi ili watu wakujue, fursa zitakuja zenyewe kwa sababu watu watajua wewe ni mtaalamu wa sheria basi utazipata fursa katika angle iyo See You At The Top Msomi!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags