Mchekeshaji Eric Omondi aachiwa huru

Mchekeshaji Eric Omondi aachiwa huru

Baada ya mpenzi wa mchekeshaji Eric Omondi, Lynne Njihia kudai kuwa polisi wamekataa kuhusika na tukio la kumkamata Omondi, hatimaye mchekeshaji huyo ameachiwa huru.

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Nairobi gossip’ ume-share picha za mchekeshaji huyo zikionesha amekiwa na mpenzi wake Lynne baada ya kuachiwa huru na polisi waliokuwa wakimshikilia.



Siku ya jana Lynne Njihia ali-shera ujumbe kupitia instastory yake kwa kudai kuwa amefika kituo cha Polisi cha Kati alichodaiwa kupelekwa Omondi baada ya kukamatwa lakini polisi wa kituo hicho wamekata kuhusika na tukio hilo.

Mchekeshaji Eric Omondi alikamatwa tena na polisi nchini Kenya, siku ya jana Ijumaa Juni 21, 2024 wakati alipokuwa kwenye maandamano yanayoendelea nchini humo ya kupinga ongezeko la kodi katika Muswada wa Fedha wa 2024/ 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags