Maua Sama Ampa Mwana-Fa Kila Kitu

Maua Sama Ampa Mwana-Fa Kila Kitu

Unaambiwa sio lazima ila ni muhimu kulipa fadhila kwa mtu aliyekusaidia na kukushika mkono kabla hujajipata. Hicho ndicho amekifanya msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama kwa msanii wa hiphop aliyemtoa, MwanaFA.

Maua Sama amefanikiwa kumlipa fadhila MwanaFA kupitia muziki mzuri kwenye kila wimbo ambao wawili hao wameshirikiana. Maua na MwanaFA wameshirikiana kwenye nyimbo kama 'Hata Sielewi' ya 2017, Gwiji ya 2020, Sio kwa Ubaya ya 2022.

Nyimbo hizo Maua amepiga viitikio na nyingine kaimba verse kabisa kitu ambacho kinampa heshima kuwa miongoni mwa wasanii waliofanya kazi nyingi na MwanaFA ambaye ni mwanamuziki na mwanasiasa anayeshikilia nafasi kama Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mbali na kushirikiana kwenye nyimbo Maua pia amehusika kutengeza Intro ya jina la 'Falsafa' ambayo MwanaFA huitumia kwenye nyimbo nyingine ambazo hajashirikiana na Maua, lakini huiweka Intro hiyo kama sehemu ya utangulizi.

Historia ya wawili hao kufahamiana ilianza baada ya Maua Sama kurekodi moja ya wimbo wake wa mwanzoni So Crazy mwaka 2013. Ambapo kupitia rafiki yake Maua aliwatumia wimbo huo wasanii kama Alikiba, Ommy Dimpoz na Ben Pol ila ni MwanaFA pekee aliouelewa. Ndipo wakarudia kuurekodi na ulipotoka ukamtambulisha Maua Sama vizuri kwenye ramani ya muziki.

Hata hivyo, licha ya Maua kurekodi wimbo huo, huko nyumbani kwao Moshi ila alipokuja Dar es Salaam na kukutana na MwanaFA, waliamua kwenda kuurudia kwa Marco Chali ambaye ni mshindi wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards 'KTMA' kama Mtayarishaji Bora 2008.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags