
Hii Ndiyo Sababu, Foby Kuangua Kilio Mechi Ya Stars
Ni wazi kuwa mtanange wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024, unaendelea kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Licha ya mashindano hayo kuendelea na kupokelewa vizuri na shabiki mwanamuziki wa Bongo Fleva Foby amezua gumzo kutokana na video yake inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akiangua kilio wakati akiimba wimbo wa taifa kwenye ufunguzi wa mashindani hayo Agosti 2, 2025.
Kutokana na video hiyo iliyoleta mjadala Foby amesema kilichofanya alie wakati wa kuimba wimbo wa taifa ni mapenzi aliyonayo kwa Tanzania.
"Mimi naipenda sana nchi yangu, lakini nalipenda sana soka. Siyo mara ya kwanza kwangu kutoa machozi wimbo wa taifa ukiwa unaimbwa. Hata kwa Ivory Cost wakati wa mashindano ya AFCON nafikiri kamera zilinitembelea na watu walihoji mbona nalia sijui nini huwa kinanikumbuka.
"Wengine wanasema nilikuwa nalia kwa sababu sikupafomu. Lakini siyo kweli kwa sababu nilijua siku moja kabla kwa hiyo ningekuwa sina mapenzi ya kweli na timu nisingeenda kabisa kwenye mashindano lakini nikaenda,"amesema Fobby.
Mkali huyo wa vibao kama Kitanda, Muda, Bora amekanusha baadhi ya watu wanaodai kuwa huwa anaandaa watu ili wamrekodi video wakati akiangua kilio.
"Sasa hivi wanasema nimemuandaa mtu anirekodi. Lakini si kitu ambacho cha kweli sasa wajiulize na zile video za Ivory Coast je niliwaandaa watu wa uwanjani? Ni hisia za kweli na mapenzi ya kweli kwa nchi yangu ndiyo zinafanya nilie.
"Hata wakati naandaa wimbo wa Taifa na Twiga Stars nilikuwa natumia kipaji changu kuwafanya mashabiki wawe wazalendo. Kwa sababu tulikuwa hatuipendi timu yetu ya taifa mimi nikionaga kitu kama vile nilikuwa nachukia nikaanza kutengeneza nyimbo kwa lengo la kuhamashisha timu zetu nalipenda soka,"amesema.
"Kwa sasa sitaki kuzungumzia kuhusiana na kwanini sikupafomu. Kwa sababu sitaki kuzua taaruki mimi ninachoweza kusema watu tufokasi na mashindano ya CHAN. Mimi hata nyimbo huwa nafanya kwa gharama zangu hakuna mtu anayeniagiza lakini ikija pesa nitapokea,"amesema.
Leave a Reply