Mike Tyson Kuchora Tattoo Usoni Sababu Ni Hii

Mike Tyson Kuchora Tattoo Usoni Sababu Ni Hii

Bondia maarufu duniani, Mike Tyson ambaye anatambulika pia kutokana na tattoo kubwa aliyonayo upande wa kushoto wa uso wake. Anadai halikuwa wazo lake kuchora tattoo ya namna hiyo bali ulikuwa ushauri wa mchora tattoo.

Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu mwenye umri wa miaka 59, kabla ya pambano lake 2013 dhidi ya Clifford Etienne. Aliweka wazi kuwa mwaka 2003 aliingia kwenye studio ya mchoraji wake wa tattoo, Victor Perez na kuomba amchore tattoo za kopa nyingi upande wa kushoto wa uso wake ili aweze kujulikana kama mtu wa mioyo kama ajiitavyo msanii wa Bongo Fleva, Jux 'King of Heart'.

Hata hivyo, mchoraji huyo alipinga wazo hilo kutoka kwa Tyson na kumshauri aondoke kisha baada ya siku kadhaa atakuwa amepata Idea ya kumchora .

Siku mbili baadaye mchora tattoo alimpigia simu na kumwambia tayari amepata wazo la kumchora, wazo ambalo lilikuwa muundo uonekanao hivi sasa ukiwakilisha kabila la 'Maori.'

Ubunifu huo kutoka kwa mchoraji huyo ulimfurahisha Tyson ambaye kwa mujibu wake anasema tattoo hiyo husimama kama kielelezo cha hali yake ya juu ya ushujaa.

Tyson anasema aliipenda idea hiyo ya muonekano wake wa tattoo. Mara nyingi hufikiria ingekuwaje kama angechora tattoo ya makopa mengi katika uso wake, anaona kama angekuwa amefanya maamuzi mabaya, hivyo mara zote amekuwa akimshukuru mchoraji wake, Victor Perez kwa ushauri huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags