Baada ya mwanamuziki Juma Jux kuitikisa Nigeria kwa sherehe ya harusi na mkewe Priscilla. Sasa sherehe nyingine inatarajiwa kufanyika Mei 28,2025 hapa nchini.
Harusi hiyo inayowahusisha Priscilla Ajoke Ojo (binti wa mwigizaji maarufu wa Nollywood, Iyabo Ojo) na mwanamuziki, Juma Jux, imekuwa gumzo barani Afrika.
“Tumemaliza Nigeria tunajiandaa na JP2025 Tanzania Super Dom, Mei 28, 2025,” amesema Ommy Dimpoz mmoja wa mastaa waliohudhuria kwenye sherehe zote za harusi ya Jux zilizofanyika nchini Nigeria.
Utakumbuka wawili hao walifunga ndoa yao ya kwanza nchini Tanzania, Februari 7,2025 ndoa ambayo ilihudhuriwa na watu wachache wakiwemo ndugu wa karibu pamoja na wasanii kama vile Diamond Platnumz, Zuchu, S2kizzy, Abba, Ommy Dimpoz na wengine.
Mahusiano ya Jux na Price yalianza mapema Agosti 2024 huku penzi lao likiteka mitandano ya kijamii baada ya Jux kwenda ukweni nchini Nigeria.
Priscilla Ajoke Ojo alionekana kwa mara ya kwanza na Jux July 19,2024 kwenye moja ya kumbi za starehe zilizopo jijini Dar es salaam. Na hii inakuwa ndoa ya kwanza kwa wapenzi hao wawili.
Jux amewahi kuwa kwenye na mahusiano na mastaa mbalimbali akiwemo Vanessa Mdee, Karen huku miaka ya nyumba akihusishwa kutoka kimapenzi na mwanamitandao kutoka Kenya, Huddah Monroe.

Leave a Reply