Mwanamuziki kutoka Nigeria, Wizkid ameripotiwa kuwa mmoja wa wasanii ambao muziki wao unajiuza wenyewe bila kiki wala matangazo yoyote.
Katika moja ya mahojiano aliyowahi kuyafanya Wiz aliweka wazi kuwa anachukizwa na kiki na matangazo. Huku akiamini ubora wa muziki wake unatosha kuvutia mashabiki.
“Sitaki kelele, sitaki drama muziki wangu unaongea wenyewe. Promo yangu ni utulivu na ubora wa kazi. Sipendi kiki, sipendi kuigiza maisha. Sipendi kuzunguka kwenye media naamini kazi yangu ndiyo matangazo yangu,”alisema Wiz
Aidha msanii huyo aliongezea hilo katika ngoma zake kama ‘Holla at Your Boy’, ‘Ojuelegba’, na ‘Joro’ akisisitiza kwamba hana haja ya kelele au drama ili aweze kufanikiwa katika muziki.
Mbali na Wizkid mastaa wengine ambao muziki wao unatembea bila promo wala kiki ni Maleek Berry, Adekunle Gold (mume wa msanii Simi) na wengine.

Leave a Reply