Simba Aitwa Tajiri Baada Ya Kumwaga Maokoto Jp2025

Simba Aitwa Tajiri Baada Ya Kumwaga Maokoto Jp2025

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Diamond amepokea maua yake huku akitajwa kuwa msanii tajiri Afrika na kuwazidi mastaa wakubwa na wenye majina kutoka Nigeria.

Kwa mujibu wa mchekeshaji kutoka nchini humo Deeone (Starboy Of Comedy) ameweka wazi kuwa kutokana na kitendo cha Simba kumwaga maokoto kwenye harusi ya Jux na Priscy kumemfanya aamini kuwa mastaa wa Nigeria hawamzidi utajiri Diamond.

“Sikuamini kama wasanii wa East Africa wana pesa kiasi hiki katika maisha yangu, hii sio kelele tu! ni pesa kweli kwani amekuja kwenye harusi ya Jux & Priscilla na kutumia zaidi ya dola 350,000 (tsh milioni 939/=).

“Sio wasanii wa huku wanakuahidi na bado hawakupi kitu, wasanii wa Nigeria itabidi muwe wapole, kuna pesa upande mwingine wa Africa, ebu tazama Waafrika Mashariki wakimwaga cash, sikuamini kabisa hii kwa Diamond, hata meno yake ya diamond (almasi) ni og, sio hawa wasanii wetu kutwa kufeki maisha tu,” amesema comedian deeone (swipe).

Utakumbuka kuwa wakati wa sherehe ya kitamaduni ya JP2025 msanii Diamond alionesha ukubwa wake kwa kuwatunza maokoto ya kutosha maharusi hao huku akionekana kutembea na begi lililojaa hela.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags