Lundenga azikwa makaburi ya familia Kidatu Morogoro

Lundenga azikwa makaburi ya familia Kidatu Morogoro

Mwili wa aliyekuwa mratibu wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, umezikwa leo Aprili 22,2025 katika makaburi ya familia, Kidatu, mkoani Morogoro. 

Mazishi ya Lundenga yamefanyika saa 6.00 mchana na kuhudhuriwa na wakazi wa maeneo ya Kidatu, Mkamba, Nyandeo na maeneo mengine ya jirani.

Mbali ya wakazi wa maeneo hayo, wadau wa masuala ya mashindano ya urembo kutoka Dar es Salaam na mikoa ya Pwani na Morogoro pia wameshiriki katika mazishi hayo.

“Tumezika salama na sasa tunarejea Dar es Salaam kuendelea na matanga,” amesema Yason Mashaka ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania enzi ya Lundenga.

Lundenga alifariki dunia Aprili 19, 2025 katika hospitali ya Kitengule iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya homa ya mapafu.

Kwa mujibu wa mkewe aitwaye Twigy Hashim ameiambia Mwananchi kabla ya kufikwa na umauti mumewe alikata kauli kwa miezi minane.

“Ukweli ni muda mrefu alikuwa amekata kauli. Yapata miezi minane ila kabla ya miezi hiyo, alikuwa anasisitiza kwamba ikitokea umauti umemkuta akazikwe nyumbani. Lakini pia alikuwa anasisitiza kwamba tuwaangalie watoto wetu ili wawe na maadili mema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags