Jamie Foxx, mwigizaji na mchekeshaji kutoka Marekani amekanusha vikali uvumi na madai ya kuwa mwanamuziki Sean “Diddy” Combs alijaribu kumuua mwaka 2023.
Jamie amekanusha hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiana na ‘The Hollywood Reporter’, akieleza kuwa Diddy hahusiki kabisa na ugonjwa uliyokuwa ukimsumbua wa kiharusi kilichosababishwa na kutokwa na damu kwenye ubongo.
“Kwa sasa niko na afya njema kabisa na kuhusu uvumi wa kuwa Diddy alihusika na kile kilichonitokea. Hapana, Puffy hakujaribu kuniua,”alisema Jamie
Mbali na hilo lakini pia aliwahi kuzungumza kuhusiana na kuhusiaka kwenye sherehe nyumbani kwa Diddy ambapo alikata kuwa alikuwa sehemu ya sherehe hizo zinazohusiana na kesi ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono.
Jamie anasema nyakati zote alizokuwa akienda aliwahi kuondoka mapema na kwa sasa amejitenga na Diddy kufuatia madai mazito yanayomkabili.

Leave a Reply