Filamu kuhusu maisha ya aliyekuwa Mfalme wa Pop wa Marekani, Michael Jackson, iitwayo ‘Michael’, imeripotiwa kuwa haitatolewa mwaka huu kama ilivyotangazwa awali, hii ni baada ya kutokamilika kwa baadhi ya matukio muhimu ya utayarishaji wake.
Inaelezwa kuwa huenda filamu hiyo ikagawanywa katika sehemu mbili, kufuatia kurejea kwa timu nzima katika eneo la kurekodia kwa ajili ya upigaji picha wa ziada, ambao unatarajiwa kudumu kwa siku 22.
Filamu hiyo, inayoongozwa na Antoine Fuqua huku mhusika mkuu akiwa ni mpwa wa Michael, Jaafar Jackson, inaripotiwa kuwa na urefu wa zaidi ya masaa matatu na nusu jambo linaloifanya kuwa ndefu kupita kiasi kwa muktadha wa filamu moja.
Sehemu ya kwanza ya filamu hiyo inadaiwa kumalizika katika kipindi ambacho Michael Jackson aliachana rasmi na kundi la Jackson 5, baada ya kutoa albamu yake maarufu ya Off the Wall.
Awali, filamu hiyo ilipangwa kutoka Oktoba 2025, lakini kutokana na mabadiliko haya ya upigaji picha na urefu wa filamu, hivyo basi filamu haitatolewa mwaka huu huku vyombo vya habari mbalimbali vikidai kuwa huwenda sehemu ya kwanza ikatoka mwaka 202

Leave a Reply