Harmonize Asherehekea Kufikisha Views Bilion Moja

Harmonize Asherehekea Kufikisha Views Bilion Moja

Msanii wa Bongo Fleva Harmonize amefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara bilioni moja kwenye mtandao wake wa Youtube.

Harmonize alianza kuweka maudhui ya muziki kwenye channel yake ya YouTube mwaka 2015 kwa kuweka wimbo wake wa kwanza 'Aiyola' uliomtambulisha kwenye ramani ya muziki.

Harmonize amefanikiwa kupandisha maudhui zaidi ya 900 kwenye mtandao wa YouTube ambapo ni jumla ya nyimbo zake, show, na mtindo wa maisha.

Mafanikio hayo yanamfanya msanii huyo kuungana na wasanii wengine barani Afrika ambao wamefanikiwa kufikisha namba kubwa ya watazamaji kwenye jukwaa hilo akiwemo Diamond Platnumz, Burna Boy, WizKid, na wengine wengi.

Utakumbuka, mwaka 2020 msanii Diamond Platnumz naye alifanikiwa kufikisha watazamaji bilioni moja wa jumla kwenye video zake za YouTube na kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Afrika mashariki kufikia mafanikio hayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags