Mwigizaji Coletha apozwa na suruali aliyovaa kanisani

Mwigizaji Coletha apozwa na suruali aliyovaa kanisani

Mwigizaji Coletha Raymond amewajia juu wanaomkosoa kwa kwenda kanisani huku amevaa suruali.

Mwigizaji huyo ambaye alichapisha video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha anatoka kanisani Jumapili ya Machi 9, 2025 huku amevalia suruali ya kitambaa na shati jeupe la mikono mirefu, amejikuta akipokea maoni ya kushambuliwa kutoka kwa mashabiki yakiponda uvaaji wake.

Akizungumza na Mwananchi leo Machi 19, 2025 Coletha amesema maneno ya watu wa mtandaoni hayamuumizi kichwa badala yake anaishi anavyotaka yeye.

"Mimi sioni shida kwa sababu nilivaa bwanga kubwa sana. Mambo mengine ni maumbile tu ya watu sikuchora sehemu zangu za siri, ningechora ningesema haileti picha nzuri. Kwanza vazi langu halileti utamanishi kwa picha yoyote ile kwa sababu wapo wanaovaa vibaya zaidi ya mimi nilivyovaa.

"Pili imani yangu vazi halinipeleki mbinguni matendo nitayofanya ndiyo yatanipeleka. Mbinguni hatutaenda kwa mavazi, wapo wanaovaa mpaka ninja lakini wadhambi, sisi hatutakiwi kumuhukumu mtu yeyote yule anayepaswa kuhukumu ni Mungu. Niliingia mpaka kanisani sasa hao watu wa mtandaoni ni kina nani yani alafu mimi na life style yangu siendeshwi na watu wa mitandaoni,"amesema

Amesema kwa alichofanya angekuwa amekosema angeomba msamaha lakini kwa kuwa hakukosea hana haja ya kumuomba mtu msamaha.

"Hayo ni maneno ya watu wa Insta ambao maamuzi ya watu maarufu wanayatoa wao, wanashindwa kuendesha maisha yao. Mimi nimetoka ndani familia yangu imeniona vizuri nipo sahihi wengine ni wa ziada. Mimi navaa suruali ambayo hainichori mimi sioni kama navaa utupu ningekuwa hivyo si kanisani nigerudishwa shida kuna masekretari wengi wa Mungu mtaani, mimi nipo tofauti sana nimelichukulia mauzauza,"amesema

Baadhi ya maoni ya mashabiki

"Nguo yako haifai katika nyumba ya ibada. Kweli unajua unarusha rusha maboga wachungaji unawapa vishawishi halafu ulivyoshindikana umepost kweli dhambi ukiizoea unaihalalisha hadharani,"

"Kanisani kwetu ukija hivyo hauingiiii,"

"Coletha usiwe mkaidi hata kama tunatenda dhambi nyumba ya ibada iheshimu,"

"Coletha mwenye hekima na upendo akionywa jambo anakuwa mpole na kutafakari, ila ukimjibu mtu hivi mnakiwa mnafanana wote, kwa heshima ya kristo tulijenge kanisa kwa upendo,"






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags