Mwigizaji wa filamu nchini Salim Ahmed 'Gabo Zigamba' leo Mei 13, 2025, amesema filamu ina nafasi kubwa ya kutoboa kimataifa kuliko muziki.
Gabo ameyasema hayo leo Mei 13, 2025, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa tamthilia yake mpya ya Baraluko na kusema kuwa tasnia ya filamu ni sanaa inayoeleweka mataifa yote.
"Muziki na filamu chepesi kufika kimataifa kama waandaaji wa filamu wataamua ni filamu. Filamu lugha yake ni kama mpira vinafanana mpira wa Barcelona na wa Bongo bado uleule. Sema tuu inategemea mmeanza wapi na filamu pia ina lugha moja.
"Tofauti na muziki, leo ukipafomu ukiacha Singeli hatukuelewi, lakini Singeli hiyo hiyo ukiipeleka sehemu fulani kuna watu wanaweza kuwa hawaielewi, lakini kwenye filamu huku mtu anaelewa hata kikorea," amesema Gabo.
Gobo amesema kwa mara ya kwanza anaenda kutumia mtandao wa Youtube kama jukwaa la kuoneshea tamthilia yake ya Baraluko ambayo itaanza kuruka kuanzia Mei 14, 2025 kwenye mtandao huo.
"Tamthilia ya Baraluko itaonekana kwenye YouTube Channel ya Gabo Zigamba, kwa muda mrefu nimekuwa sijihusishi sana na mitandao ya kijamii, kwahiyo uongozi umekaa ukaamua niweze kurudi ili niendane na vitu ambavyo vinaendelea. Mara nyingi tumekuwa tunalisha filamu kwenye majukwaa mengine kwahiyo tumeona tusiiache pia jukwaa la YouTube.
Amesema anaiweka katika jukwaa hilo ili kuwafikia mashabiki ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kuangali Television. Pia amesema kasi ya dunia kwasasa ipo kwenye simu za mkononi na namba za watazamaji wa TV imepungua.
"Kuna namna watu wengi wanapitwa na baadhi ya kazi zetu kwasababu watu wapo bize sana maofisini kwahiyo vitu vingi mara nyingi wanakuwa wanatazama kwenye simu. Lakini pia kuna utamaduni wa kukaa kwenye Tv unapangua namba zinapungua haifanani mwanzo na sasa kwahiyo kiu yetu ni kutomuacha yeyote kati ya mashabiki zetu haina tafisri mbaya isipokuwa ni kuendelea kujikuza.
Amesema tamtilia yake ya Mawio aliwashtua wengi baada ya kuwatumia wasanii wa muziki wa Bongo Fleva ambao ni Barnaba na Isha Mashauzi lakini kwenye Baraluko ametumia wachezaji wa Mpira wa miguu.
"Sijachukua msanii wa Bongo Fleva safari hii nimewachukua wacheza mpira na wameigiza japo kila mmoja anandoto zake lakini kuna wacheza mpira wanapenda kuigiza na kuimba kwa hiyo wapo watu wawategemee," amesema Gabo.
Tamthilia ya Bararuko imechezwa na waigazaji tofauti tofauti akiwemo Gabo Zigamba ambaye ndiye muhusika mkuu, Zulfa Msomali ambaye kwenye tamthilia hiyo anafahamika kama Annabela, Marry Mawigi na wengine wengi huku ikionesha maisha ya Ndoa, Familia, Usaliti, Changamoto za Mahusiano

Leave a Reply