Drake Aweka Rekodi Billboard

Drake Aweka Rekodi Billboard

Msanii nguli wa Hip Hop kutoka Canada, Drake, ameweka historia mpya katika tasnia ya muziki duniani kwa kuwa msanii wa kwanza kuwahi kuingia kwenye orodha ya juu ya Billboard Top 10 mara 82.

Rekodi hiyo mpya imevunja rekodi zote zilizowahi kuwepo, na imethibitisha hadhi ya Drake kama mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa zaidi katika historia ya muziki wa kizazi hiki.

Tangu kuanza kwake muziki mwaka 2009, Drake ameendelea kutamba nyimbo zenye mafanikio makubwa kama "God’s Plan", "Hotline Bling", "In My Feelings", na "One Dance", ambazo nyingi zimepanda hadi nafasi ya kwanza kwenye chati hizo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Billboard, Drake ameingia katika chati hizo kwa kuwazidi rapa wote akiwemo Lil Wayne aliyeingia mara 27, Nick Minaj 24, Eminem mara 24, Kendrick Lamar mara 23, Jay Z 22, Ye 21, Ludacris 18, Travis Scott mara 18 na Savage mara 17.

Licha ya mambo yake kutokwenda sawa kwa mwaka uliyoisha kutokana na bifu lake na Lamar lakini mashabiki wameendelea kumsapoti msanii huyo huku wengi wao katika mitandao ya kijamii wakimpongeza kwa hatua hiyo kubwa aliyofikia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags