Drake Awajia Juu Waliyomkataa Wakati Wa Bifu Lake Na Lamar

Drake Awajia Juu Waliyomkataa Wakati Wa Bifu Lake Na Lamar

Rapa kutoka Marekani Drake amewachana watu wake wa karibu waliyomkataa wakati wa bifu lake na msanii mwenzake Kendrick Lamar.

Drake amewatolea uvivu watu hao kupitia wimbo aliyoshirikishwa na Conductor Williams kwa kueleza kuwa alikatishwa tamaa kwa jinsi ndugu zake walivyomgeuka.

“Ulimwengu ulipenda, hata ndugu zangu walipata tiketi, ilionekana kama walipenda kila dakika yake. Jua tu kwamba hili jambo ni la kibinafsi kwetu na halikuwa tu biashara. Kuchanganua tabia za watu ni jambo linaloshuku kidogo,” anaimba Drake

Aidha kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa watu ambao Drake amewalenga waliokuwa marafiki zake wa karibu ni pamoja na LeBron James na Demarde Rozan ambao walihudhuria kwenye tamasha la Lamar lililopewa jina la ‘Pop Out’ lililofanyika Juni mwaka jana.

Bifu la wawili hao lilianza katikati mwa mwaka 2024 baada ya Lamar kutoa ngoma iitwayo ‘Like That’ akijitambulisha kuwa yeye ni bora kuliko Drake huku akidai kuwa amewazika mastaa wote wanaomuunga mkono Drake kupitia albumu yake ya ‘For All The Dog’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags