Msanii wa maigizo na mfanya biashara Jackline Wolper amemjia juu Mwijaku kwa kumtaka aache kuongelea maisha na biashara yake kufuatia taarifa za kuachana na alie kuwa mumewake Rich Mitindo.
kupitia ukurasa wake wa instagram Wolper ameandika akiwataka watukuacha kuzungumzia kama kiki inshu ya kuachana na aliekuwa mumewe Rich Mitindo huku akimtaja Mwijaku kuwa miongoni mwa watu hao.
"Kwa mliozoea kiki kwenye ishu za watu kwenye hili nita deal na mmoja mmoja Mwijaku sheria naijua vizuri basi njoo Taratibu najua Rich ni rafiki yako sana na katika pitapita zangu za chati nawewe umo kutumana basi tuheshimiane usiongelee kabisa biashara yangu na maisha yangu kama mahakama unajua vizuri chunga unachoongea" ameandika Wolper.
Chapisho hilo nikufuatia hapo jana Wolper kutangaza kuachana na aliekuwa mumewake Rich Mitindo ambapo aliweka wazi kupitia ukurasa wake wa instagram akieleza kuwa yupo kwenye mchakato wa talaka japo mpaka sasa Rich hajathibitisha kuachana kwao.
Leave a Reply