A Father Figure yatimiza mwaka mmoja

A Father Figure yatimiza mwaka mmoja

Leo ni Birth Day ya album ya A Father Figure kutoka kwa mkali wa Hip Hop Dizasta Vina ambayo ilitoka rasmi January 6, 2024 ikiwa imeshiba ngoma kama Theluji, Nobody is safe 5, Hatia VI, Not A Hero, Chupa Moja Ya Ziada, Karibu Duniani, Wachezaji Wa Tmu, Top Shelf, Fanani, Mbuzi, Achia Jala na zingine nyingi.

Muundo wa mashairi aliyo tumia kwenye album ya AFF unajumuisha usimulizi wa matukio ngoma kama Achia Jala, Not A Hero na Wachezaji Wa timu, Hadithi za maisha halisi ya jamii anayotokea ngoma kama Theluji, Tungo zake zinasifika kwa kuelimisha na kugusa masuala ya kijamii kama vile malezi ngoma kama Karibu Duniani, siasa, umasikini ngoma kama Get Better, Dini ngoma kama Hatia VI, haki na usawa, Misimamo ngoma kama Fanani na Top Shelf na masuala mengine ndani na ulimwengu mzima kwa ujumla.

Hii inatajwa kuwa miongoni mwa album bora sio tu kwa mwaka 2024 bali mashabiki wanaihusudu mpaka kuitaja kuwa album bora ya Hip Hop kwa muda wote bongo, japo haija sambaa sana kwa sababu hakuamua kuiweka kwenye Digital platform na badala yake anaiuza kupitia Watsap na Email shilling 10000 kwa kila nakala 1 ya Album.

A Father Figure hii ni album ya tatu kutoka kwa Dizasta Vinna ikitanguliwa na A Verteller na Jesusta, Mabali na hapo anatajwa kuwa ndie msanii pekee tanzania mwenye Squels zaidi ya moja ambazo ni Hatia, Comfession na Nobody Is Safe yote hayo imeyafanya kabla ya kufikisha miaka 30, Bila kuwa na usimamizi, Bila msaada na bila kuwa na mkataba kwenye studio ya kurekodia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags