Bob Marley Alivyompatia Maokoto Ya Kudumu Rafiki Yake

Bob Marley Alivyompatia Maokoto Ya Kudumu Rafiki Yake

Miongoni mwa nyimbo kubwa za Bob Marley ni pamoja na hii ya ‘No Woman No Cry’ iliyotoka 1974 ikiwa moja ya ngoma zinazo patikana kwenye album yake ya Natty Dread.

Kabla ya Bob Marley kuuachia wimbo huo alimuweka rafiki yake Vincent Ford kama mwandishi mwenza wa wimbo wake wa No woman No Cry, ambapo kwa wakati huo Ford alikuwa anajihusisha na Biashara ya kuuza supu mji wa Trench sehemu aliokulia Bob Maley.

Na hii ndio sababu ya Bob Marley kumuweka Vincent Ford kama muandishi mwenza kwenye wimbo huo.

Bob alifanya uamuzi huo ili Ford awe sehemu ya watu wanaopokea mirabaha (Mauzo) ya kazi hiyo ili aendeleze biashara hiyo ya supu ambayo ilikuwa inasaidia kwenye mitaa aliokulia Bob, na kusadia biashara hiyo kuendelea kwa zaidi ya miaka 30.

Uamuzi huo ulipelekea Bob kuingia mzozo wa kimkataba na kampuni ya K man Music iliyokuwa ikisimamia uchapishaji wa kazi zake kwa kumuandika Ford lakini hawakufanikiwa kwani tayari Ford alikuwa akitambulika kama muandishi mwenza wa kazi hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags