Hakuna Ushahidi Wa Kumkamata Nicki Minaj

Hakuna Ushahidi Wa Kumkamata Nicki Minaj

Ombi lililowasilishwa la kumkamata rapa Nick Minaj kufuatiwa na kesi ya kumpiga aliyekuwa meneja wake wa zamani, limekataliwa kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kutosha

Msemaji wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kaunti ya Wayne aliiambia TMZ kuwa wamepitia ombi kutoka kwa Idara ya Polisi ya Detroit la kumkamata msanii huyo lakini wamelikataa kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha unao thibitisha uhalifu huo kutendeka.

Utakumbuka kuwa Nicki anakabiliwa na madai ya kumshambulia aliyewahi kuwa meneja wake Brandon Garrett nyuma ya jukwaa la Little Caesars Arena, Detroit wakati wa ziara ya masanii huyo ya Pinky Friday II April, 2024.

Hata hivyo, ofisi ya Mwendesha Mashtaka imewataka idara ya polisi wa Detroit kufanya uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags