Rapa kutoka Marekani ameonesha ukarimu wake kama baadhi ya mastaa wanavyoonesha kwa mashabiki wao, kwa kumpatia muhudumu wa baa aitwaye Renee Brown, dola 20,000 ikiwa ni zaidi ya Sh 49.6 milioni.
Malone wakati alipokuwa kwenye matembezi ya likizo yake ya mwisho wa mwaka alipitia katika baa iitwayo Railyard iliyopo jijini Houston na kuona jinsi Renee anavyochapa kazi usiku na mchana bila kupumzika.
Aidha Malone aliamua kumkabidhi pesa mwanadada huyo baada ya kusikiliza kwa makini historia yake ambapo alikuwa akifanya kazi kwa bidii ili kutengeneza maisha yake upya baada ya kukumbana na changamoto mwanzoni mwa mwaka 2024.
Leave a Reply